Picha | Ijue Hoteli Kubwa Ya Afrika Ambayo Wanaishi Maskini

Mwaka 1955 kwenye mji Beiran nchini Msumbiji kulijengwa hotel iliyojulikana kama Grande Hotel, Hoteli hiyo ilijengwa kwenye pwani ya masumbiji ilikiwa lengo ni kuwavutia wageni waliotembelea nchi hiyo iliyokua chini ya koloni la Ureno.
Ilipojengwa ilikua ni moja kati ya Hoteli kubwa Afrika, wamiliki walipendekeza kuweka sehemu ya kuchezea kamari lakini walinyimwa kibali kutoka kwa maafisa wa ureno.
Licha ya kujengwa ukanda hoteli hiyo haikuwavutia wageni hivyo ilifungwa mwaka 1963 kama hotel na badala yake  kutumiwa kwa sherehe kubwa peke yake.
Mwishoni mwa miaka ya 70 ilitumika kama kambi ya jeshi na gereza la wanasiasa
Miaka kumi baada ya hotel hiyo kufungwa wakimbizi walianza kukimbilia hatolini hapo.


Wakazi wa Grande hotel hawalipi kodi na sheria waliyoipitisha hawaruhusu mgeni kuingia kwenye jamii yao kwa madai kuwa hotel imejaa.

Sehemu kubwa ya hoteli hiyo haina umeme hivyo kumetawaliwa giza na joto kali huku miundombinu ya jengo hilo ikiwa ni mibovu.


Imefika hatua miti imeanza kuota juu ya jengo hilo hivyo kuanza kuharibu baadhi ya maeneo ya jengo hilo.
Kumetengenezwa sehemu ya burudani ya kutizama filamu katika sehemu ya pekee ilo na umeme katika hoteli hiyo. kwa kawaida kuna watoo na watu wazima wanaokaa kutizama TV 

Baadhi ya familia sasa wanaishi katika hoteli hiyo kwa vizazi vitatu. miaka 24 tangu kumalizika vita zaidi ya idadi nusu ya raia Msumbiji wanaendelea kuishi katika umaskini.
 
Lipo baraza maalum ambalo hukutana kila mwezi kujadili mienendo ya wakazi na matatizo yao. Michezo pia ni moja kati ya vitu vinavyopewa kipaum,bele.

SOURCE: BBCSwahili.
Post a Comment
Powered by Blogger.