Mwongozaji wa Video, Nisher atoa Kitisho kizito


Muongozaji wa video nchini, Nisher amedai kuwa amelazimika kuwa kimya makusudi ili kujiandaa kuja na ujio wa awamu nyingine akiwa na nguvu zaidi.

 Nisher amesema hapendi kufanya vitu kawaida  ila anataka kufanya vitu vikubwa na atarudi kwa kishindo kisicho cha kawaida kwenye soko.

“Right now I’m taking my time kidogo,” amesema Nisher kueleza kwanini ghafla amekuwa kimya tena. “I’m coming out with something big, ila nipo kwenye, so sio kitu cha haraka. Kwa upande wangu right now, I’m not about releasing kazi kila siku,” amesisitiza.

“I’m all about big moves basi. I do something big na chill nafanya mambo mengine na return na hit zingine na chill sababu kwa sasa nina mambo mengi sana kwenye sahani yangu, na kujigawa sana inakuwa kazi so na balance,” ameongeza.


Hata hivyo ametoa hofu mashabiki wake kuwa amefanya hivyo kuisuka upya akaunti yake. 

“Ninalaunch upya page yangu ya Instagram,” anasema. So watu wakiona hamna posts wasipanic, nailaunch upya ili iwe versatile zaidi for my marketing purposes.”

“Itakuwa na ubora zaidi picha nzuri zaidi na pia watu wataweza kunipata kiurahisi zaidi ili kuepukana na matapeli.” na amesisitiza kuwa account yake haijaibiwa (hacked) ila anaifunga kwa muda.

Nisher kwa sasa yupo nchini Afrika Kusini.
Post a Comment
Powered by Blogger.