Mmiliki Wa Facebook Na Instagram Mark Zuckerbug Azitembelea Nchi Hizi Za Afrika


Mmiliki na mwanzilishi wa kampuni inayomiliki mitandao ya Facebook na Istagram na bilionea raia wa Marekani, Mark Zuckerberg amezuru katika nchi za Nigeria na Kenya katika ziara ya inayotajwa kuwa ya kushtukiza ambapo akiwa nchini Nigeria alikukutana na mastaa mbalimbali nchini humo  akiwemo Yemi Alade, Basket Mouth, Dj Cuppy na wengine,huku lengo rasmi la ziara ya bilionea huyo mwenye utajiri unaokadiriwa kufikia kiasi cha dola bilioni 54.4,likiwa ni kuwawezesha vijana katika mpango wake wa kuwasaidia wajasiriamali wachanga.
                      Zuckerberg akiwa na mastaa nchini Nigeria.
Alienda nchini humo kwa kushtukiza Jumanne hii na kutembelea kituo cha masuala ya teknolojia huko Yaba mjini Lagos. Kulikuwa na ulinzi mkali na wengi kwenye kituo hicho kiitwacho CcHUB, hawakujua kama atawatembelea.
 "Ni mara yangu ya kwanza kuja Afrika chini ya jangwa la Sahara. Nitakutana na watengenezaji na wajasiriamali na kujifunza kuhusu mwenendo wa makampuni machanga,” taarifa hiyo iliandikwa kwenye akaunti yake ya  mtandao wa Facebook.Licha ya kutembelea kituo hicho cha mafunzo ya teknolojia Zuckerberg alitembea kwenye mitaa ya jiji la Lagos bila ulinzi wa kutosha ambapo pia alionekana akifanya mazoezi kwenye daraja la Lekki Bridge nchini humo. Mark Zuckerberg (kushoto)akijumuika  kupata chakula na maafisa wa Taasisi ya Habari na mawasiliano nchini Kenya.
Post a Comment
Powered by Blogger.