Miaka 28 Ya Wema Sepetu, Zifahamu Hizi Dondoo Chache Kuhusu Yeye.


Takribani miaka kumi sasa tangu Tanzania tuanze kulisikia jina la mrembo Wema Sepetu hii ilikuja mara baada ya ushindi wake wa taji la Miss Tanzania mwaka 2006.
Wema Sepetu aliiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Miss World nchini Poland kwa bahati maya hakuweza kuingia fainali za kinyang’anyiro hicho.
Licha ya kushindwa kwenye fainali hizo Mrembo Wema hakuwahi kuchuja wala kupoteza umaarufu wake zaidi ya kutengeneza vichwa vya habari kila kukicha.
Baada ya kuachana na ishu ya Miss Tanzania moja kwa moja Wema Sepetu alijiingiza kwenye uigizaji  kwa ushawishi wa aliyekua nguli wa filma za kibongo Marehemu Stephen Kanumba.

Filamu alizowahi kuigiza ni pamoja na:
A Point of No Return
2008 – Family Tears
2009 – Red Valentine
2010 – Sakata
2010 – White Maria
2010 – Tafrani
2011 – 14 Days
2011 – Lerato
2011 – Basilisa
2011 – The Diary
2011 – DJ Ben
2012 Crazy Tenant
House Boy
It Was Not My Fault
2014 Madame
2015 Mapenzi Yamerogwa
Saa Mbovu
Chungu Cha Tatu
2016 Family
Mbali na uigizaji Wema pia ni mjasiriamali na mmilili wa kampuni ya uzalishaji wa filamu ya Endless Fame,
Leo septemba 28 mrembo Wema Sepetu anasherehekea siku yake ya kuzaliwa,
seetheafrica.com inaungana na mashabiki na wapenzi wa Wema Sepetu katika kusherehekea nae siku hii muhimu.
Post a Comment
Powered by Blogger.