Mambo Saba Ya Kumjua Mwanaume Mwenye Nia na Mwanamke


mahusiano na wanaume ambao hawaonyeshi kama wananaia ya dhati ya kuwa na mahusiano ya kudumu  bila ya wao kutambua.

Wengi wao hujiaminisha zaidi kwa wanaume hao ambao huamini kuwa pengine huweza kuolewa nao ,bila kujua kuwa baadhi ya wanaume ni waharibifu .

Kwa kulitambua hilo,chini ni tabia 7 kuu za mwanaume ambaye anania ya dhati ya kutaka kuishi na wewe na ikiwezekana akuoe kabisa.
 
1. Anakupigia simu mara kwa mara na kukuuliza siku yako imeendaje. Anafanya hivi kirafiki na kwa upendo, haigizi. Anakupenda kweli.
 
2. Anakutembelea mara kwa mara, anakuwa karibu na wewe kipindi unaumwa, hii inamaanisha kwamba yupo tayari kukuvumilia katika shida na raha. Mpende mwanaume huyu.
 
3. Anawapenda ndugu zako kama ndugu zake. Anaongea nao vizuri na kusaidiana mambo ya hapa na pale. Mtizame kwa jicho la tatu huyu mwanaume!
 
4. Anaongea na wewe kwa adabu na kwa upole, anakukosoa bila wasiwasi kama kuna mambo unaenenda visivyo. Anakuelekeza njia zilizonyoka..sio wa kumuacha huyu!
 
5. Hakulazimishi kufanya mapenzi. Anakupenda sana kiasi kwamba hawezi kukulazimisha jambo ambalo hauko na hiari nalo. Yupo karibu na wewe wakati wote na sio tu anapokutaka kimapenzi, huyu ni bonge la bwana.
 
6. Anakusaidia fedha pale unapokua umekwama kabisa, yuko na jukumu la kukusaidia kiuchumi. Anapenda kukupa kile ambacho amejaaliwa nacho. Hana mkono wa birika, Huyu anakupenda!
 
7. Anazungumzia future yake na wewe, mipango ya baadae pamoja na wewe, huyu anayo dhamira ya dhati kutoka moyoni mwake ya kukufanya uwe mkewe.

Hizi ni moja ya dalili kwamba mwanaume wako anakupenda na anataka atengeneze future pamoja na wewe. Usikate tamaa juu ya mwanaume wa aina hii
Post a Comment
Powered by Blogger.