Kocha Wa Uingereza Sam Allardyce aacha Kazi Baada ya Kutoa Siri.


Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza Sam allardyce, ameachia ngazi kwa makubaliano na Shirikisho na mpira wa miguu nchini humo baada ya kufanya kazi kama meneja wa timu hiyo kwa muda wa siku 67 na kucheza mechi moja tu


Moja ya sababu zilizosabaisha kuondolewa kwenye nafasi hiyo ni ushauri alioutoa wa kupindisha sheria za usajili wa wachezaji. Pia kocha huyo mwenye umri wa miaka 61 anashutuma za kosa la kutumia madaraka yake kuingia makubaliano yenye dhamani ya £400,000 sawa na 1,138,942,650 shilingi za kitanzania na Far East firm.

Chama cha michezo cha uingereza FA kimesema Sam allardyce tabia yake haikuwa nzuri, na kumtaka atakae chukua nafasi yake kwa muda kuwa ni Gareth Southgate
FA waliendelea kusema “amekubali kuwa amefanya kosa na ameomba msamaha, haya siyo maamuzi mepesi bali kipao mbele cha FA ni kulinda maslai mapana ya michezo na kudumisha nidhamu ya hali ya juu kwenye mpira wa miguu(Soka)”

“kama kocha wa timu ya Taifa ya uingereza lazima awe na uwezo wa kuonyesha uongozi bora na pia awe ni mtu mwenye intergrity kwenye michez wakati wote”.

Kwa kusema hivyo Sam allardyc amekuwa ni moja wa kocha aliyeifundisha timu hiyo kwa muda mfupi zaidi kwa kuifundisha timu ya Uingereza kwa muda wa siku 67 tu.

Post a Comment
Powered by Blogger.