Kingine Kipya Unachotakiwa Kukijua Wewe Mtumiaji Wa Snapchat


Kampuni ya Snapchat imezindua miwani inayomuezesha mtu kurekodi video na kuisambaza katika mtandao huo wa kijamii.
Inasema miwani hiyo iliyopewa jina 'Spectacles', inanasa kumbukumbu za watu kupitia kamera ndogo na itauzwa kwa dola 130 sawa na 286,000 za kitanzania.

Snapchat imejiongezea sifa kwenye mitandao ya kijamii inayotumiwa kutuma ujumbe, zikiwemo picha na video ambazo hufutwa baada ya kuonekana mara moja.
Lakini kifaa hicho kipya na kampuni hiyo kubadilisha jina kutoka Snapchat na kujiita Snap, zinadhihirisha azma ya kampuni hiyo kupita kiwango cha kuwa mtanadao wa ku chati.
Katika tangazo lake la biashara, Snap inasema miwani hiyo ya kutuma video ina lensi ya ukubwa wa digri 115, iliyo na upana zaidi kuliko kamera za smartphones.

Na ina uwezo wa kurekodi video kwa hadi sekundi kumi kwa mara moja.
Picha hizo zinaweza kutumwa moja kwa moja kwenye mtandao huo wa kijamii ili mtu aweze kuzisambaza kwa watumiaji wengine wa mtandao huo.

Post a Comment
Powered by Blogger.