Mh Temba Kurithishwa Majukumu Ya Fella.Mkurugenzi wa Mkubwa na Wanae Foundation pamoja na Yamoto Band, Mkubwa Fella amesema tayari ameshampata mtu sahihi ambaye atamwachia mikoba yake ya kusimamia wasanii pale atakapostaafu.

“Kusema kweli mtu ambaye nitamwachia kijiti ni Temba, tayari imeshamuandaa vya kutosha na bado naendelea, kwa hiyo Temba tayari anaelewa nini anatakiwa kufanya muda ukifika,” alisema Fella.

Kwa upande wa Temba amesema yupo tayari kupokea majukumu atayoachiwa na bossi wake huyo.

“Mimi nipo poa tu, tayari nimeshazungumza naye kuhusu ili swala na naamini kila kitu kitaenda sawa,” alisema Temba.

Pia Temba alisema hata kama akiwa kwenye jukumu la umeneja hataacha kufanya muziki kwa kuwa muziki ni sehemu ya maisha yake.


HII HAPA VIDEO YA TEMNA NA FELLA WAKIPIGA STORI NA HZB TV

Post a Comment
Powered by Blogger.