Fahamu Umuhimu wa Mifuko ya Pics Katika Utunzaji naUhifadhi Wa Mazao


Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi imekuwa ikifanya jitihada za kupunguza upotevu wa mazao nchini kupitia program na mipango mbalimbali itakazo saidia upatikanaji wa mazao ya kutosha kwa biashara na chakula.

Pamoja na jitihada za serikali za kuongeza uzalishaji wa mazao hapa nchini kwa kutumia mikakati na mipango mbalimbali kutoka tani milioni 9.99 mwaka 2005/6 hadi tani milioni 16.01 mwaka 2014/15, bado upotevu wa mazao baada ya kuvunwa ni tatizo kubwa hususan mazao ya nafaka amapo kwa mwaka hufikia asilimia 30 hadi 40.

Upotevu wa mazao umekua ukisababisha nchi kutokuwa na chakula kutosha nahata kipato cha wakulima kupungua na hivyo huchangia pato la Taifa hushuka hali ambayo huipelekea nchi kua tegemezi.


Chuo kikuu cha Purdue kwa kushirikiana na kiwanda cha Pee Pee Tanzania Limited (PPTL) kilichopo Tanga – Tanzania kimeleta teknolojia mpya “mifuko ya tabaka tatu” ijulikanayo kwa jina la PICS yenye ujazo wa kilogram 100 ambayo imefanyiwa utafiti na wataalamu wa taasisi ya utafiti ya ukiliguru na chuo kikuu cha sokoine (SUA) ambayo inatajwa kua ni suluhisho la upotevu wa mazao.

Utafiti huo umefanywa na Profesa Rodes Makundi kwa kushirikiana na Profesa Apia Masawe wa chuo kikuu cha kilimo (SUA) umeonyesha sio tu mazao yatakuwa salama yakiwa ndani ya mifuko hiyo bali hata wadudu wanaobangua mazao hufa baada ya siku kadhaa bada ya kukosa hewa wanapokua ndani ya mifuko hiyo

Mifuko ya tabaka PICS imetengenezwa mahsusi kwa teknolojia ya “hermetic” yaani isiyopitisha hewa, hivyo kuwanyima hewa ya oxygen wadudu ambao ni viumbe hai wanaohitaji hewa kuendelea kuishi pasi na kuwekewa sumu.

Wataalamu hao pia waliongeza kuwa mifuko hiyo yenye kisalfeti nje na mifuko miwili ya nailoni nzito, matumizi yake ni lazima mazao yawe yamekauka vizuri, ili kuzuia wadudu wanaoharibu mazao kwa kunusa ikiwamo panya.

Abubakar Mshana mmoja wa wakulima mwenye ushahidi wa kutumia mifuko ya PICS ameeleza kuwa mwezi wa nane 2014 alihifadhi mazao yake kewnye mifuko hii bila kuyawekea dawa huku yakiwa na wadudu ndani ili kuthibitisha kama kweli hayatameng’enywa ambapo mwezi wa tatu 2016 alikuta mazao yake yakiwa katika usalama na wale wadudu wakiwa wamekufa. 

Mradi wa Mifuko ya PICs ililetwa nchini Tanzania mwezi Julai mwaka 2014 na Chuo Kikuu cha Purdue - Indiana, Marekani kwa kushirikiana na kiwanda cha PPTL kilichopo Tanga, na ilizinduliwa rasmi katika ukumbi wa bunge mnamo tarehe 13 June 2016 na Naibu spika wa bunge la Jamhuri wa muungano Mheshimiwa Dokta Ntulia Hudson.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wabunge pamoja na mawaziri akiwemo waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mheshimiwa Charles Mwijage na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa William Ole Nasha.

Teknolojia hii imeweza kutumika kwa takriban miaka tisa katika nchi za Afrika magharibi na baada ya mafanikio makubwa katika nchi hizo mradi huu umesambazwa katika nchi saba ambazo ni Malawi, Uganda, Ethiopia, Nigeria, Ghana, Burkina Faso na Tanzania.
Post a Comment
Powered by Blogger.