Coke Studio Kuwaunganisha Yamoto Band Na Muethiopia Lij Michael


Kundi la Yamoto Band lipo jijini Nairobi, Kenya kuiwakilisha Tanzania kwenye kipindi maarufu cha Coke Studio Africa. Wataonekana kwa mara ya kwanza kwenye show hiyo mwaka huu kwa kuungana na msanii wa Ethiopia, Lij Michael, aliyejipatia umaarufu kwa wimbo ‘Zaraye yehun nege’ ambaye pia anashiriki kwa mara ya kwanza kwenye msimu wa nne wa Coke Studio Africa.

Wasanii hao wanatarajiwa kujumuisha ladha za Bongo na vile vya hip hop ya Ethiopia, huku wimbo wao ukitayarishwa na producer wa Ufaransa,  DSK (asili yake ni Ivory Coast).

Akiongelea kushiriki kwa mara ya kwanza, msanii wa kundi hilo,  Enock Bella alisema, “Naishukuru Coke Studio Africa kwa kutuamini na kutupa fursa kushiriki kwenye kipindi kuonesha uwezo wetu katika hatua hii ya mwanzo ya muziki wetu. Tunafurahia kufanya kazi na Lij Michael na tunategemea kuchanganya muziki wa Bongo Flava na muziki kutoka Ethiopia,” na kuongeza, “Studio na utayarishaji upo katika ukubwa ambao hatujawahi kuuona kabla na tuna hamu kubwa.”

Lij Michael pia aliisifia Coke Studio Africa akidai kuwa mabadilishano kati ya Yamoto Band na yeye ni ya kupendeza. Akiweka wazi kile mashabiki wanapaswa kungojea, alisema “Mtayarishaji wa mdundo DSK alitupa ladha kama za mdundo wa asili ya Tanzania na wakati huo huo nimepata mdundo halisi wa nchi yangu ya Ethiopia. Pindi show ikianza, tazamieni tumbuizo la uhakika – itakuwa ya moto.”

Yamoto Band na Lij Michael watakuwa wenyeji kwenye ukurasa wa Facebook wa Coca-Cola kuanzia saa nane mchana Alhamis hii, Septemba 1. Usikose kutazama kuwaona live. Watajibu pia maswali yako kuhusu safari zao kimuziki. Andika swali lako kupitia @CocaColaAfrica na weka hashtags: #AskYamotoBand #AskLijMichael #CokeStudioAfrica

DSK ni mongoni mwa watayarishaji wa muziki Afrika kwenye kipindi cha msimu huu na amepewa jukumu ya kuzifanyia kazi mchanganyiko wa muziki uliochaguliwa kutoka zaidi ya nchi kumi na mbili. Wengine ni pamoja na Madtraxx (Kenya), Bushingtone (Uganda), Masterkraft (Nigeria), Chopstix (Nigeria) na Maphorisa (Afrika Kusini).

STELLINA MWENDA - GIVE ME THAT MONEY (MUSIC VIDEO)

Post a Comment
Powered by Blogger.