Video Tano Za Bongo Zinazofanya Vizuri Mtandaoni.Kwenye #TheTop5 jumanne ya Agosti 23 nimeamua kukupa orodha ya Video tano za muziki wa bongo zinazofanya vizuri mtandaoni kwa mujibu wa takwimu za YouTube.


5:Fid Q Ft/ Christian Bella - Roho

Agosti 13, ndio siku rasmi Fid Q aliwapa mashabiki wake kibali cha kukiona kichupa hiki akiwa ameshirikisha mkali wa masauti Christian Bella, Ndani ya siku kumi tangu ipandishwe youtube Roho imeangaliwa zaidi ya mara 175,390.

 

 4:Christian Bella - Nishike. Jamaa alitokea pande za Congo mpaka Bongo kuwaonyesha wabongo kile ambacho Mungu amemtuma kukileta, Tangu kuanza kwake ni miaka kumi sasa Christian Bella hajawahi kushuka kimuziki zaidi ya kupaa zaidi. Hii hapa ni ngoma yake mpya Inaitwa nishike, Imekamata nafasi ya Nne kwenye video zinazofanya vizuri Bongo kwa kutazamwa zaidi ya mara 300,850 ndani ya siku 19.

 3:JayPryzah Ft. Diamond Platnumz - Watora Mari Mukudzeyi Mukombe ambae mimi wewe tunamjua kama Jay Pryzah ni mshikaji kutokea kitaa cha Zimbabwe alidondoka Bongo moja kwa moja mpaka Studio za Wcb Wasafi, Producer Laizer Classic akatengeneza mdundo ambao uliwaunganisha Jay Pryzah na CEO wa WCB (Diamond Platnumz). Mzigo umeangaliwa zaidi ya mara 758,670 ndani ya siku kumi na moja. 

2: Dully Sykes Ft/ Harmonize - Inde. Hakuna ubishi kama Inde ndio ngoma kubwa kibongobongo pengine na nchi za jirani,Ni mdundo mwingine tena kutoka kwenye mkono wa Laizer Classic wa WCB unawaunganisha Brotherman Dully Sykes na mtu mbaya Harmo mwenye Nize zake (Harmonize)kwenye kichupa hiki tangu kuachiwa kwake Agosti 11 mwaka huu Inde imetazamwa zaidi ya mara 853,790. 

 Chegge Ft/ Diamond Platnumz - Waache Waoane Ni Chegge Chigunda kwenye kolabo yake na Diamond Platnumz kwenye namba 1 ya video 5 za Bongo zinazoendelea kufanya vizuri mtandaoni tangu agosti 4 mwaka huu Waache Waoane imetazamwa zaidi ya mara 1,046,690.

Post a Comment
Powered by Blogger.