YAJUE MAMBO 6:MAKUBWA YA RAIS KAGAME NA RAIS MAGUFULI WALIVYOZUNGUMZA LEO.


Rais wa Rwanda Paul Kagame leo amewasili nchini Tanzania ambapo pamoja na mambo mengi atakayoyafanya katika ziara yake hii, atafungua rasmi maonyesho ya 40 ya biashara ya kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam leo jioni saa 10.

Aidha, majira ya saa saba Rias Paul Kagame na Rais John Pombe Magufuli walipata wasaa wa kuzungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari kutoka Ikulu jijini Dar es Slaam. Yafuatayo ni baadhi ya mambo mengi waliyoyazungumzia.

Ujenzi wa reli ya kisasa (Standard gauge) kutokea Dar es Salaam hadi Kigali.
  Rais Magufuli kama alivyowahi kusema awali, leo amesema kuwa reli hiyo itakuwa ni ya kisasa na itasaidia usafirishaji wa mizigo na usafiri kutoka Tanzania hadi Rwanda. Aidha, Mawaziri husika wa miundombinu kutoka pande zote mbili watakutana hivi karibuni ili kuweka mjengo kazi kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi huo mara moja.

Bandari ya Dar es Salaam. Rais Magufuli ameeleza kuwa takribani asilimia 70 ya bidhaa zza Rwanda hupita katika bandari ya Dar es Slaam.

 Aidha ameeleza kuwa kulikuwapo na vikwazo mbalimbali katika ufanisi wa bandari hiyo ambavyo kwa sasa hivimo. Katika hatua nyingine Rais Magufuli amesema kuwa serikali itatenga sehemu ya kuhifadhi mizigo yote ya Rwanda mara inapotolewa bandarini ili kupunguza mloloongo uliopo.

Pia Rais Magufuli amesema kuwa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) itajenga kituo kimoja nchini Rwanda ili kuwasaidia wafanyabaishara wa Rwanda kupunguza mlolongo wa kuja kufanya malipo Tanzania na badala yake wanaweza kufanya wakiwa Kigali.

Usafirishaji wa mizigizo kwa njia ya barabara. Rais Magufuli kama alivyoeleza awali alipokuwa nchini Rwanda, leo amesema tena kuwa, sasa vituo vya kupimia mizigo kwa magari vitakuwa vitatu tu toka Dar es Salaam hadi Rwanda. Hii itasaidia kupunguza usumbufu uliokuwapo mwanzoni kwa magari hayo ya mizigo.

Ununuzi wa ndege mbili kubwa. Katika sekta ya usafirishaji, Rais Magufuli alisema kuwa alipewa ushauri na Rais Kagame juu ya namna ya kupata ndege na sasa serikali kwa kushirikiana na watalaam kutoka Rwanda Air wapo katika mchakato wa kununua ndege hizo na alisema kama mipango yote itakwenda sawa basi mwishoni mwa mwezi Septemba ndege hizo zitawasili nchini.

Suala la Dimplomasia kati ya Tanzania na Rwanda. Akizungumzia hili, Rais Kagame alisema kuwa, lengo kubwa la ujio wake ni kuhakikisha anakuza umoja baina ya nchi hizi mbili ili kuweza kuleta maendeleo katika nchi zote.

 Kwa upande wa Rais Magufuli amesema kuwa Tanzania na Rwanda zina uhusiano wa kihistoria na kueleza kuwa wanaamini pamoja wanaweza kusonga mbele.

Ujenzi wa kituo kimoja cha kukusanyia mapato nchini. Rais Kagame alimueleza Rais Magufuli kuwa licha ya uwapo wa makampuni mbalimbali yanayokusanya kodi Rwanda, lakini kuna kituo kimoja cha serikali ambacho hufuatilia kwa karibu makusanyo hayo na kuisaidia serikali kuhakikisha hakuna mtu anayeiibia serikali.

 Hivyo Rais Magufuli alisema kuwa atapokea msaada wa wataalamu kutoka Rwanda ili kushauri namna ya ujengjia wa kituo hicho kitakachofuatilia namna kila kampuni inavyokusanya mapato ili kuongeza mapato ya serikali.

Rais Magufuli alisema sasa kuna makampuni mengi ambapo kila moja lina namna yake ya kukusanya mapato kitu ambacho kinapelekea serikali kupoteza fedha ku kukosa filisofia moja inayoeleweka kati zoezi la ukusanyaji mapato.
Post a Comment
Powered by Blogger.