Wasanii Wa WCB Wanabebwa Na Promo,Hakuna Anayenizidi:Abdul Kiba.

Abdul Kiba.
Abdu Kiba amesema kuwa promotion ndiyo inawabeba wasanii wa lebo ya WCB.
Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM, “Sijafikiria kuimba na msanii kutoka WCB, kwa sababu sijaona anayeimba type ya muziki wangu.”
“Hata kama wana promote kwa sababu ndiyo walipoona wao ndiyo wanaweza wakafanya na watu wakaweza kuelewa lakini siku zote ajuae hazami,” alisema Abdu Kiba.
Aidha aliongeza kuwa bado hajaona msanii anayeimba type ya muziki wake ndani ya lebo hiyo [WCB].
Hata hivyo mapema mwezi huu msanii huyo alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio kuwa yupo tayari kujiunga na lebo wa WCB kama watakubaliana na kuweka hela mezani kauli ambayo baadaye yeye mwenyewe aliipinga kuwa watu hawakumuelewa vizuri alichomaanisha.


Post a Comment
Powered by Blogger.