WAFUASI WA WASSIRA WAKATA RUFAA.
Wafuasi wa aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini, Steven Wassira wamembwaga mahakamani mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Ester Bulaya wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika rufaa yao ya kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu kutupilia mbali kesi yao.
Wafuasi hao, Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Escietik Malagila walifungua kesi ya uchaguzi kupinga ushindi wa Bulaya katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 wakijitambulisha kama wapiga kura.
Hata hivyo  mahakama kuu kanda  ya mwanza katika uamuzi wake uliotolewa na jaji Mohamed Gwae alitupilia mbali kesi yao baada ya kukabiliana na pingamizi la wakili wa Bulaya, Tundu Lissu kuwa hawakuwa na haki kisheria kufungua kesi hiyo.
Kutokana na uamuzi huo walalamikaji hao walikata rufaa mahakama ya rufani na wakati wa usikilizwaji wa rufaa hiyo waliieleza mahakama hiyo kupitia kwa wakili wao Yassin Membar kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 111 (1) (a)  cha sheria ya uchaguzi ya mwaka 2010 wana haki ya kufungua kesi hiyo.
Post a Comment
Powered by Blogger.