Wabongo Wametajwa Sana Tuzo Za Africa Entertainment Huku Diamond Na Alikiba Sahani Moja.

KIWANDA cha burudani nchini kinazidi kukua na kuchukua sura mpya kila siku, jana tuzo kubwa duniani za African Entertainment Awards USA (AEA USA 2016), zimetangaza majina ya wasanii watakaowania tuzo kwenye vipengele mbalimbali na mwaka huu Bongo inawakilishwa na mastaa 12.
Miongoni mwa majina yaliyochomoza kwenye tuzo hizo zitakazotolewa Oktoba 31, huko New York, Marekani ni msanii Diamond Platnumz ambaye ametajwa kuwania vipengele vitano ambavyo ni Video Bora ya Mwaka, Msanii Bora wa Kiume Afrika, Wimbo Bora wa Mwaka na Kolabo Bora ya Mwaka kupitia wimbo wa Zigo alioshirikiana na AY.
Millard Ayo, naye ametajwa kuwania tuzo ya Bloga Bora Afrika, Harmonize anawania tuzo ya Msanii Bora Chipukizi, Rayvan, anawania tuzo ya Kipaji Bora Kipya na Joh Makini anawania tuzo mbili ambazo ni Msanii Bora Hip Hop Afrika na Video Bora ya Mwaka.
Wasanii wengine ni Vanessa Mdee anayewania tuzo ya Wimbo Bora wa Mwaka, Linnah Sanga, anawania tuzo ya Msanii Bora wa Kike Afrika, Ali Kiba na Christian Bella kupitia wimbo wao unaoitwa Nagharamia wanawania tuzo ya Kolabo Bora ya Mwaka, Yamoto Band nao wanawania tuzo ya Kundi Bora la Mwaka huku Dj Ommy akiwania tuzo za DJ Bora Afrika.
Njia rahisi ya kuwapigia kura mastaa hawa ni kupitia tovuti yao ambayo ni www.aeausa.net au ukatembelea kwenye kurasa za mitandao yao ya kijamii ili kupata njia nyingine za kuwapigia kura.
Post a Comment
Powered by Blogger.