Video | Mwanamuziki Wa Bongoflava Aliyetekwa Na Rafiki Wa Instagram

Ni msichana mdogo anayevutia kwa sura na hata kwa umbo,mpole wa sura na muonekano pia na anayekuja kwa kasi katika tasnia ya music hasa katika music wa zuku,bongo fleva aliyepitia mengi ambayo mwingine angekutana nayo asingeweze kuvumilia labda angejiua au angefanya kitu kibaya zaidi katika nchi hii ya Tanzania hakika Sabra Mathew(Jolee) anahitaji kupewa hata kombe la kuwa mwanadada mvumilivu kwa kila jambo alilopitia maishani ni staa wa bongo na kama kawaida kwa kupitia mtu maarufu tunajifunza mengi...jifunze kupitia Jolee( Sabra mathew). Amezaliwa katika familia ya jumla ya watoto watatu na yeye akiwa msichana pekee katika familia hiyo na mtoto wa pili kwa mzee Mathew na hii ndo tarehe aliyozaliwa 16\6\..huko mkoani Arusha baba yake akiwa ni mfanya biashara na mama yake mwalimu wa shule binafsi, Jolee kwa kabila ni Muarusha aliyechanganyikana na mnyatulu,shule ya msingi alisoma merelani na sekondari Arusha day kwa bahati mbaya hakuweza kufaulu kidato cha nne kwasababu tu yakuvunjika kidole kwa kipigo kikali alichapigwa na kaka yake baada ya kumuhisi anamahusiano wa kimapenzi na mtu fulani wakati akiwa bado shuleni. maisha yake ndipo yalipoaza kuwa ya changamoto baba yake alikataa kumsomesha huku akimuambia labda ampe mtaji wa nyanya auze hali iliyomfanya ajisikie vibaya ikiwa pamoja na yeye kusomesha ndugu zake ambao walifeli kabisa shule ndipo alipoamua kuondoka nyumbani na kuaza maisha kwa rafiki yake ambaye alikuwa mama ntilie huko Arusha kwa kipindi kifupi baada ya rafiki yake kujua kuwa si mtu ambaye anategemea wazazi wake aliamua kumuita ndugu yake na kumuambia anabidi ahame nyumba waliyokuwa wanaishi kwasababu tu yakumuondoa kwasababu hana hela. kwa bahati nzuri katika pitapita zake za sokoni alikutana na rafiki yake mwingine na kuonba waishi wote nyumba ambayo walikuwa wasichana watatu kwa kuhama kwake kwa rafiki yake haikuwa sababu ya yeye kuacha kufanya kazi ya kuwa mpishi na pia muhudumu mnzuri kwa wateja hali iliyomfanya apendwe na wengi ikiwemo baba mmoja mwalimu wa sekondari ya shule ya sekondari aliomba amsaidie katika biashara zake za kutengeneza kitimoto siku zilisonga na kusonga zaidi lakini kama mwenyezi Mungu anataka kukupitisha sehemu fulani ili uwe mtu fulani basi kwa hili kwa Jolee kufukuzwa tena nyumbani alipokuwa anaishi na rafiki kwasababu tu ya kukataa kuwa na muuza duka ambaye alikuwa anawaonga wadada hao kwa kujua siku moja hata pata tunda kwa bibie,

Angalia Hapa Video Ya Jolee - Dua Yangu katika siku isiyozaniwa wakati anarudi nyumbani huku akiwa anajifikiria suala nzima la kwenda kumsaidia mama huyo biashara yake na kuishi naye nyumbani kwa kitu alichokiona mbele yake wakati ambao amewasili nyumbani hakuamini alikuta nguo zake zikiwa zimetupwa kwa kuzagaa hali iliyomfanya ajisikie vibaya kwa kujua tu sababu ya kumkataa mwanaume yule ndo yamesababisha yote hayo kukosana na rafiki zake na kukosa pa kuishi. Lakini Mungu si Athumani wala Ramadhani akili ilimjia kumpigia mwana baba huyo ambaye alimuitaji kufanya naye kazi na akaamua kumpigia ili amuambie hali halisi na kuona hata msaidie lakini kwa bahati nzuri jibu alilopewa ni kuchukuliwa pale na kwenda kuishi na mama pamoja na mume wake huyo kama mtoto kutokana tu na nidhamu na juhudi zake za kazi. Japo kuwa kwa maisha aliyoaza kuyaishi kipindi akiwa tokea na umri wa miaka kumi na saba(17) baba yake hakuamini na kumwambia hakika ataangaika na kurudi nyumbani alipotoka japo hakuamini maneno hayo na kuzidi kutafuta ili atoke zaidi katika maisha yake,alifanya kazi kwa miezi kadhaa na kuona anaitaji kuaza maisha yake yeye mwenyewe bila kumtegemea mtu ni kwasababu tu yakukua akili aliaza taratibu kununua godoro,nk ambavyo ni muhimu nyumbani japo hakuwa ata na aliaza kutafuta chumba na hatimaye kupata lakini siku zilipita na chumba alichohitaji kukamilika lakini hakuwa ata na shilingi kumi yakulipia siku ya kwenda kuangalia nyumba hiyo ilipita kwani hakujua anaenda kufanya nini bila hela siku ilipita na jua lilipochomoza kwa kukaribisha siku mpya baba yake mzazi alimtumia hela ambayo hakutegemea bila kupoteza muda alienda kulipia chumba baada ya siku kadhaa aliona ni bora kuwaambia walezi wake kuwa anahitaji kujitegemea suala ambalo liliwaumiza na hawakuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana naye kwa shingo upande, baada yakuaza kujua anahitaji kuondoka kwa wakati ambao washamzoea kama mtoto wao kumzaa. Alikutana na dada mmoja aliyeitwa stellah katika biashara yake ya kitimoto dada huyo alikuwa anaduka ambalo alihitaji kufanya kazi na mrembo huyu kitu ambacho alifurahi na kumfanya aombe wazazi wake ruhusa ya kuacha kazi hiyo na kupiga hatua zaidi ya maisha. Stellah aliyekuwa na mchango mkubwa sana katika maisha yake aliye muita "malkia wa nguvu" aliyempa kila kitu na ata kumfanyia birthday pale aliposahau siku hiyo kubwa ya kuzaliwa kwake,japo ambalo hatosahau baada ya dada huyo kufufua ndoto yake iliyozimika ghafla kama mshumaa ya kuwa mtangazaji bora duniani kukubali kumsomesha na kumlipia ada yote mpaka alipo maliza elimu yake ya cheti katika chuo cha Safari college mkoani moshi Maisha katika jiji la Dar es salaam yalianzia hapo na pamoja na kuwa na saloom Yombo ambayo baba yake ndiye aliyemuwezesha zaidi katika biashara hiyo na ndipo alipoaza kutoa nyimbo yake ya kwanza ya Usinihukumu ambayo ilipigwa sana Capital,Itv,Bongo 5 kama mwenzi na kuchangia kwa marafiki zake kwa kupost nyimbo hiyo na kuamua kuingia Studio kutoa nyingine kama Nakuhitaji,Dua yangu ambazo zimegusa sehemu ya maisha yake kwa nafasi fulani na nyingine zikiwa njiani kwa kutoka na kutamba sana mitaani,Jolee hapo ndipo ulipoazia umaarufu wake katika nchi ya tanzania naye akiwa kama mtanzania mzalendo. Jolee aliwahi kutekwa na watu asiwajua na mpaka leo hajui sababu ya kutekwa na ni tukio iliyompelekea kuangaika na kujikuta kuwa alitupwa Bagamoyo kwa kutokea tabata alipochukuliwa na mmoja wa shabiki zake kutoka katika mtandao wa kijamii wa instagram kushindwa kupewa Rb na polisi wa Dar kwani Rb alibidi akate bagamoyo na ndicho kitu au tukio asilolisahau ikiwemo na kushikwa na polisi usiku wa saa tano akiwa anatokea kwenye sherehe ya rafiki yakena polisi walisema wamemshika kwa kosa la kutembea usiku kwa jinsi isivyo halali na kusema kuwa alisingiziwa Malengo yake na sifa zake ni kuwa Mtangazaji bora Afrika Mashariki,pia mwimbaji bora wa kike katika muziki wa zuku na bongo fleva...anapenda kupika na kukaa peke yake pia kuogelea kubwa zaidi ni mchezaji mnzuri wa kikapu, anajivunia kwa kutokuwa na tattoo yoyote katika mwili wake pia kutopigana na mtu yeyote hawezi kuwa na kisilani na mtu na kuwapenda watu wote ambao wako pamoja katika soko la muziki bongo.. Kama hukuangalia video yake ya Dua YanguTazama hapa.
Post a Comment
Powered by Blogger.