Ugonjwa Wa Ukimwi Kujadiliwa Leo.

Mkutano wa kimataifa kuhusu maambukizi ya virusi vya ukimwi na ukimwi unaanza leo mjini Durban,Afrika kusini ukiwa na lengo la kuongeza harakati za kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi. Takwimu za maambukizi kwa ujumla imeshuka lakini bado kuna watu wapatao milioni thelathini na sita wanaishi na virusi vya ukimwi vinavyosababisha Ukimwi.
Nchi hiyo ilipata sifa kubwa katika vita dhidi ya UKIMWI miaka ya 90 ambako kasi ya maambukizi ilipungua.
Mwaka wa 2013 takriban watu zaidi ya milioni moja Unusu walikuwa wakiishi na virusi vinavyosababisha UKIMWI na katika kipindi hicho watu laki sita na elf tatu walifariki kutokana na magonjwa yanayohusiana na UKIMWI.
Post a Comment
Powered by Blogger.