TUJENGE TABIA YA KUJIFUNZA KWA MAKOSA KUTEKELEZA MIPANGO YETU.

TUJENGE TABIA YA KUJIFUNZA KWA MAKOSA KUTEKELEZA MIPANGO YETU.

Jana klabu ya Simba ya jijini Dar es salaam ilimtangaza rasmi Joseph Marius Omog kuwa kocha mkuu wa kikosi chao kwa kipindi cha miaka miwili ijayo.
Omog, kocha bora wa mwaka Afrika mwaka 2014, akiwa na medali ya dhahabu kupitia kombe la shirikisho barani Afrika akiwa na klabu ya AC-Leopards ya Congo Brazaville ametia saini kandarasi hiyo ya miaka miwili ili kukaa msimbazi hadi mwaka 2018.
Akiifundisha Azam fc Omog alipita kati kati ya Simba na Yanga kutwaa ubingwa wa Tanzania bara baada ya matajiri hao kuusotea kwa muda mrefu.
Omog anakuja Simba na rekodi zake mfukoni, kuifanya Cv yake ing'ae na hivyo kulandana na historia iliyotukuka ya wana msimbazi hao.
Bila shaka ligi ya Tanzania anaijua vema na mashindano ya Afrika anayafahamu vema hii inamfanya awe chaguo sahihi.
Lakini ili Simba wafaidi ujuzi, weledi na uzoefu wa Omog, hawana budi kujiuliza huko nyuma walikosea wapi hadi wakapotea?
Yapo mambo kadhaa ambayo endapo hawatarudia kuyafanya tutaiona Simba ikirudi kwenye ramani ya soka Tanzania.


1.Kocha apewe mamlaka kamili asiingiliwe majukumu yake kama upangaji wa kikosi, kambi, mazoezi nk.


2. Viongozi wabaki kuwa watawala na wasimamizi wa timu na siyo kuwa na mamlaka juu ya mchezaji mmoja mmoja hata kama wamemsajili kwa fedha za mifukoni mwao.


3. Viongozi wafanye mambo kwa weledi bila kukurupuka na kuendeshwa na mihemko kwa kuzingatia maslahi ya Simba.


4. Viongozi wawe makini na lugha wanasotumia dhidi ya wachezaji hata kunapokuwa na makosa, meza ya mazungumzo itumike, taratibu za maonyo kiofisi zifuatwe wajiepushe kuwadhalilisha au "kuwabwatukia" wachezaji kupitia vyombo vya habari.


5. Maslahi, matunzo na maandalizi kwa wachezaji yapewe kipaumbele kuliko kitu kingine chochote.


6. Viongozi waepuke shinikizo la matokeo na kuifanya timu isambaratike kisaikolojia.


7. Uongozi ukae chini na kutafuta namna ya kuwaunganisha wanachama,mashabiki na wapenzi wa klabu yao ili wawe na mshikamano na umoja kuipa hamasa timu yao.


Kwa upande wa mashabiki wajue kuwa kujenga timu hakuhitaji shinikizo kunataka utulivu na muda. Hivyo mashabiki wawe nyuma ya timu yao wakati wote ili kuirejesha mahali pake panapostahili.
Kwa Omog hakuna kisingizio cha vyeti wala uzoefu bali tatizo lolote litakalotokea kwa asilimia kubwa litakuwa limesababishwa na mfumo mbovu wa uendeshaji wa vilabu vyetu.


Viongozi waache maneno mengi na visingizio visivyo na msingi, wasikeshe kumtafuta mchawi wa kumbebesha lawama badala yake watilie mkazo ktk mambo ya msingi kuinyanyua upya klabu yao.
Kila la heri wekundu wa msimbazi ktk "mission" mpya kuelekea ktk mafanikio.


‪#‎Imani‬ Kelvin Mbaga
www.seetheafrica.com
Post a Comment
Powered by Blogger.