Tuhuma Za Kubaka Mbuzi Hadi Kufa:Asakwa Na Polisi.

Jeshi la Polisi nchini Kenya linamtafuta mkazi wa Kibirichi kutoka katika Kaunti ya Nyamira kwa tuhuma za kufanya ukatili dhidi ya wanyama.
Mkazi wa Kaunti hiyo anatuhumuwa kuiba mbuzi na kisha kumbaka hadi kufa. Taarifa zinaeleza kuwa mtuhumiwa huyo aliiba mbuzi na kisha kumfungia kwenye mti kabla ya kutenda kitendo hicho. Na baada ya kumbaka mbuzi huyo, mtuhumiwa huyo alitoweka kusikojulikana baada ya kuwasikia vijana wawili wanaomtafuta mbuzi huyo wakija eneo alipo.
Vijana hao hawakuweza kumtambua mtu huyo na wakati huo mbuzi huyo alikuwa amejilaza chini huku hajiwezi na ndipo vijana hao walitoa taarifa kwa wanakijiji waliofika eneo la tukio.
Post a Comment
Powered by Blogger.