Timu Ya Man City Ya Pep Guardiola Yachezea Kichapo Toka Kwa Bayern Munich.

 Kuelekea katika kujimarisha kwa msimu ujao timu mbalimbali barani Ulaya zinaendelea kucheza mechi za kirafiki kwa mara ya kwanza Pep Guardiola alirudi katika dimba la Allianz Arena akiwa na kikosi cha Man City na kupata mapokezi makubwa kwa msimu uliopita alikuwa kocha wa Bayern Munich.

Manchester City, wakicheza mechi yao ya kwanza ya kujiandaa kwa msimu mpya chini ya meneja mpya Pep Guardiola, wamefungwa 1-0  na klabu ya zamani ya meneja huyo Bayern Munich.
City walifungwa bao moja na Erdal Ozturk wa Bayern, ambao kwa sasa mkufunzi wao ni Carlo Ancelotti.
Wachezaji wengi nyota hawakucheza mechi hiyo kwani bado wanapumzika baada ya kushiriki Euro 2016 na Copa America.
Guardiola alichezesha wachezaji 12 wa timu ya vijana, mechi hiyo iliyochezewa Allianz Arena.
Mlinda lango wao alikuwa Angus Gunn, mwanawe mchezaji nyota wa zamani wa Norwich Bryan.
City sasa wataelekea Uchina ambapo watacheza dhidi ya Manchester United siku ya Jumatatu mchezo huu unatarajiwa kuwa na upinzani kutokana na kuwa na makocha wawili waliowahi kukutana nchini Hispania.
Wachezaji wengine wataungana na timu hiyo kwenda China ni pamoja na  Sergio Aguero, David Silva, Nolito, Raheem Sterling na Joe Hart ambao jana hawakuweza kucheza mpambano huu.
Post a Comment
Powered by Blogger.