TAZAMA JINSI MFANYABIASHARA ANAVYOIBIA SERIKALI MILIONI 7 HADI 8 KILA DAKIKA MOJA.

Mohamed Murtaza Yusuph Alli ni mtu aliye katikati ya tanuru la ufisadi ambapo anatuhumiwa kwa wizi wa kati ya milioni saba hadi nane kwa dakika moja. Kikubwa kinachowashangaza Watanzania wengi ni kivipi mtu mmoja anaweza kuiba kiasi kikubwa cha fedha namna hiyo kwa muda mfupi hivyo?.

Kwa mjibu wa Rais Magufuli, mtandao wa Alli unatuhumiwa kuiibia serikali kati ya milioni saba hadi nane kwa kila dakika moja kwa kutumia mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFD).

Rais Magufuli alibainisha kuwa mtandao huo wa kifisadi inahusisha wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).

Ingawa Rais Magufuli hakulitaja jina hilo moja kwa moja wakati akizungumzia sakata hili, lakini Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna Valentino Mlowola alisema kuwa Alli ndiye kinara wa mtandao huo. Kufatia kubainika kwa mtandao huo, TAKUKURU inazichunguza kampuni 300 zilizoshiriki katika tuhuma hii na ambapo 4 tayari zimekutwa na hatia ya kukwepa kodi ya bilioni 30 tangu 2010.

Alli anatuhumiwa kuzalisha risiti zilizo nje ya mfumo wa TRA na kuziuza kwa  makampuni 300 bila zenyewe kufanya biashara. Anadaiwa kuwa alikuwa akiuza risiti kwa bei ya asilimia 5 ya kodi. 

Na baada ya kampuni hizo kupata risiti hizo zilikwenda kudai mrejesho wa asilimia 18 TRA, hivyo zikawa zinaiibia serikali.

Kampuni hizo ni Skol Building Material Ltd, Farm Plant (T) Limited, A.M. Steel & Iron Mills Limited na A.M. Trailer Manufacturers Limited.

Hivyo kampuni hizo zimetakiwa hadi Julai 7 ziwe zimelipa kodi hiyo serikalini. Aidha Rais Magufuli alisema kuwa ataanzanisha kikosi maalumu cha kufuatilia matumizi ya mashine za EFD ili kuweza kubaini wale wote wanaoleta udanganyifu.

Chanzo: Nipashe
Post a Comment
Powered by Blogger.