Tazama Hapa Ratiba Ya Ligi Kuu Ya Vodacom Tanzania Bara 2016/17.

Mshikeshike wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu wa 2016-2017 utakaoshirikisha jumla ya timu 16 kuanza rasmi mwezi wa nane tarehe 20.
Ligi hiyo inayosimamiwa na shirikisho la soka Tanzania [TFF] kwa udhamini wa kampuni ya simu ya Vodacom na Azam Media kabla ya ufunguzi Augusti 20,itatanguliwa na mechi ya ngao ya jamii kati ya Yanga na Azam FC mchezo huu unatarajiwa kuchezwa August 17.
Katika mechi za ufunguzi Augusti 20,timu zitafungua dimba katika viwanja mbalimbali nyasi kuwaka moto mjini Bukoba wenyeji Kagera watakuwa Kaitaba kucheza na Mbeya City,Simb watakuwa Taifa kucheza na Ndanda na Katika uwanja wa CCM Kirumba Toto Africa watacheza Mwadui.
Katika uwanja wa Kambarage Mjini Shinyanga wapiga dembe Stand United watacheza na Mbao FC,Mtibwa Sugar watacheza na Ruvu Shooting katika uwanja wa Manungu,Songea watakuwa nyumbani katika uwanja wa Samora mjini Songea watawaalika Tanzania Prinsons na mchezo kati ya Azam dhidi ya African Lyon utachezwa tarehe 21 katika uwanja wa Azam Complex.
Mechi ya Yanga dhidi ya JKT Ruvu imepangwa kuchezwa tarehe 31 lakini wanajangwani hao watacheza tarehe 28 August na African Lyon.Kwani mechi ya mzunguko wa kwanza inapisha ratiba ya kombe la shirikisho hivyo mabingwa hao watetezi wataicheza kama kiporo kwa mujibu wa ratiba hiyo.
Timu tatu ambazo zimepanda kutoka ligi daraja la kwanza na kuingia ligi kuu ni Ruvu Shooting,African Lyon na Mbao FC.
Post a Comment
Powered by Blogger.