MSIBA:Tanzinia Ya Bongo Movie Mchekeshaji Maarufu Kundambanda Afariki Dunia.

Msanii maarufu wa Vichekesho ndugu Ismail Issa Makombe a.k.a KUNDAMBANDA,amefariki dunia usiku wa kuamkia leo kwa ugonjwa ambao ulikuwa unamsumbua wa Ini.
Kundambanda alikuwa miongoni wa wachekeshaji katika tasnia ya maigizo nchini Tanzania na pia alikuwa mgombea wa ubunge wa CUF na kwenye jimbo la Masasi Mtwara katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi wa Disemba 2015 baada ya ule wa Oktoba kutofanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa mgombea wa awali wa UKAWA Mh.Emmanuel Makaida [NLP].
Katika uchaguzi huo wa Disemba 2015 Kundambanda alipata kura 14,069 dhidi ya kura 16,597 za mshindi Rashid Chua Chua kutoka CCM.
Taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwao Masasi.
Post a Comment
Powered by Blogger.