Mwaka Moja Tangu Ben Affleck Atangaze Kuachana Na Mkewe, Wamefikia Hatua Hii


Mwezi june mwaka jana muigizaji  Ben Affleck na mke wake Jennifer Garner walitangaza kuvunjika kwa ndoa yao, Goodnews ni kwamba wawili hao wanaripotiwa kuwa pamoja mpaka leo.
Chanzo cha karibu na familia ya muigizaji Ben Affleck kilisema “Inasemekana karatasi za talaka hazikuwahi kujazwa kwa kipindi chote wamekua wakitafuta suluhisho la ndoa yao.”
Chanzo hicho kilichimba ndani zaidi na kuibua mapya kuwa Ben Affleck amekua akilala kwenye chumba cha wageni tangu kutokea kwa mgogoro wa ndoaa yao mapema mwaka jana.
Sio kitu cha kawaida kwa wanandoa kutangaza mwisho wa ndoa yao halafu wakaendelea kuishi pamoja kwa zaidi ya mwaka mmoja.
“Labda wanajaribu kufikiria watakapotengana ni jinsi gani wataweza kuishi na watoto wao watatu ambao ni Violet Affleck, Seraphina Rose Elizabeth Affleck, na  Samuel Garner Affleck. “ Kilisema Chanzo Hicho.
Post a Comment
Powered by Blogger.