SOMA HAPA TETEZI ZA SOKA ZA USAJILI ULAYA JUMATATU YA LEO.

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATATU 04.07.2016.

Kiungo wa Manchester United Juan Mata, 28, anakaribia kujiunga na Everton baada ya tetesi kusema Zlatan Ibrahimovic, 34, amepewa namba ya jezi yake (Daily Telegraph).


 Manchester United wanajiandaa kumsajili mshambuliaji wa Pachuca, Hirving Lozano, 20, atakapotoka kwenye michuano ya Olimpiki akiichezea timu yake ya taifa ya Mexico (Futbol Entre Lineas).

 Crystal Palace huenda wakamuuza Mkongomani Yannick Bolasie, 27, na West Ham wanataka kumsajili winga huyo (Daily Mirror).

 Winga wa Dinamo Zagreb, Marko Pjaka, 21, ana nafasi kubwa ya kuhamia katika EPL msimu ujao, kwa mujibu wa mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo ya Croatia. Liverpool wanamtazama mchezaji huyo (FC Internews).
 Meneja mpya wa Manchester City Pep Guardiola bado anamtaka beki wa kati wa Everton John Stones, 21, licha ya klabu yake kutaka pauni milioni 50 (Daily Mail).

 Kiungo wa Derby County, Will Hughes, 21, anatazamwa na Manchester United, wakati meneja mpya Jose Mourinho akitaka kuongeza idadi ya wachezaji wazawa katika kikosi chake (Sun).

Meneja wa Everton Ronald Koeman anataka kumsajili kipa wa Valencia Diego Alves, 31, msimu huu (Deporte Valeciano).

 Manchester City wanajiandaa kumsajii kipa Geronimo Rulli, 24, kutoka Deportivo Maldonado ya Uruguay kwa pauni milioni 7.5, ili kuleta ushindani kwa Joe Hart (Express).

 Kiungo mshambuliaji wa Real Madrid James Rodriguez, 24, anajiandaa kujiunga na Paris St-Germain (Yahoo Sports France).

Liverpool wanasema kiungo wao Joe Allen, 26, ana thamani ya pauni milioni 14. Swansea wametoa pauni milioni 8 wakimtaka mchezaji huyo aliyebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake (Daily Mail).

 Kusajiliwa kwa Michy Batshuayi, 21, na Chelsea huenda kukamfanya Diego Costa, 27, kuondoka Darajani (Daily Telegraph).

 Winga wa Manchester United Adnan Januzaj, 21, atamwambia Mourinho kuwa anataka kuondoka iwapo hayupo kwenye mipango yake ya kikosi cha kwanza (Sun).

 Beki wa zamani wa Real Madrid Alvaro Arbeloa, 33, anasakwa na Newcastle United (Football Espana).

 Meneja wa zamani wa Chelsea Guus Hiddink anataka kuzungumza na chama cha soka cha England FA, kuchukua mikoba ya Roy Hodgson (The Times).

 Meneja mpya wa Chelsea, Antonio Conte anamtaka mshambuliaji wa Southampton, Graziano Pelle, 30, (Sky Italia).

 Mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku, 23, anataka mazungumzo mapya na klabu hiyo baada ya mmiliki mpya Farhad Mori kusema mchezaji huyo ana thamani ya pauni milioni 75 (Daily Star).

 Mshambuliaji wa Manchester City Kelechi Iheanacho, 19, amekiri kuwa hatokwenda kwenye michuano ya Olimpiki baada ya klabu yake kuweka pingamizi kwa Nigeria kumuita (ESPN).

 Liverpool wako tayari kumuacha kipa kutoka Hungary, Adam Bogdan aondoke, na kujiunga na Wigan Athletic (Daily Star).

Post a Comment
Powered by Blogger.