SIMBA YATAJA SABABU ZA KUACHANA NA HAMIS KIIZA.
Katibu Mkuu wa klabu ya Simba SC Patrick Kahemele amekiambia kituo kimoja cha radio cha jijini Dar es Salaam kwamba, kutemwa kwa mshambuliaji raia wa Uganda Hamisi Kiiza kumetokana na nidhamu yake mbovu ndani ya klabu hiyo.
Kahemele amesema kamati ya usajili ya Simba imeamua kuachana mshambulizi huyo baada ya kukaanae mara kadhaa lakini hakukuwa na mabadiliko ndipo walipoamua kuchukua uamuzi wa kuachana naye.
“Mchezaji akianza kuleta manenomaneno au akianza kufanya vurugu inakuwa shida na inaweza kuharibu timu nzima. Na mwaka huu Simba imepania kufanya vizuri kwahiyo haiwezi kuruhusu virusi ndani ya klabu,” aesema Kahemele ambaye ameanza kutekeleza majukumu yake kama Katibu Mkuu wa Simba tangu Julai 1 alipotambulishwa rasmi mbele ya waandishi wa habari.
Kiiza aliifungia Simba magoli 19 magoli mawili nyuma ya Amis Tambwe mfungaji bora wa msimu na kuisaidia timu yake kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa VPL nyuma ya Azam FC na mabingwa wa ligi hiyo Yanga SC.


Post a Comment
Powered by Blogger.