Simba Yapata Pigo,Beki Kisiki Atimka.
MLINZI wa kati na nahodha wa zamani wa timu ya Simba SC, Hassan
Isihaka amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Ndanda FC ya Mtwara.
Isihaka ambaye alivuliwa majukumu ya unahodha wakati ligi ikiendelea msimu uliopita kutokana na kumgomea kocha Jackson Mayanja kuingia uwanjani katika mchezo wa hatua ya 16 bora katika michuano ya kombe la FA dhidi ya Singida United.
Isihaka alimuuliza Mayanja ‘Kwanini haukunichezesha dhidi ya Yanga na kunipanga katika mechi dhidi ya Singida?’
Yalikuwa ni makosa ambayo hakuna aliyekuwa upande wake. Klabu ilimfungia kwa muda wa mwezi mmoja na aliporejea hakuwa mchezaji muhimu tena.
Alipoteza nafasi yake kwa kijana Novatus Lufunga. Kujiunga kwake na Ndanda kunaweza kumpa nafasi ya kucheza na kujiimarisha upya.