SERIKALI KUBORESHA JWTZ ILI KUKABILIANA NA UHALIFU.Serikali kuboresha Mafunzo ya kukabiliana na uhalifu kwa JWTZ ili kuifanya Tanzania nchi ya usalama,waziri wa ulinzi  na JKT Dr.Hussein Mwinyi amesema hayo wakati akifungua mafunzo ya askari kutoka nchi kumi duniani ya jinsi ya kukabiliana na uhalifu 

Dr.Mwinyi amesema kasi ya uhalifu duniani kwa sasa ni kubwa hivyo Tanzania kama ni taifa ni lazima ishirikiane na mataifa mengine kuithibiti hali hiyo.


Mkuu wa mafunzo hayo Brigedia jenerali yohana maboko amesema kupitia mafunzo hayo Askari wa Tanzania watapata utaalamu zaidi kutoka nchi zilizoendelea ikiwemo Marekani jinsi ya kukabiliana na uhalifu kisasa zaidi.
 
Mafunzo hayo ya wili mbili yamehusisha Askari zaidi ya mia mbili kutoka nchi kumi na taasisi tatu za kimataifa.
Post a Comment
Powered by Blogger.