RAIS WA GAMBIA APIGA MARUFUKU NDOA ZA UTOTONI.

Rais wa Gambia President Yahya Jammeh amepiga marufuku ndoa za watoto , limeripoti shirika la habari la AFP .
Limeripoti kuwa alitangaza marufuku hiyo siku ya Jumatano akisema:
''Yeyote atakaemuoa msichana mwenye umri wa chini ya miaka 18 ataishi jela mika 20. Wazazi wa msichana watatumikia kifungo cha jela miaka 21 na yeyote ambae anafahamu na kushindwa kutoa taarifa kuhusu suala hili atafungwa jela miaka 10''
Rais Jammeh metishia pia kuwafunga jela ma Imam wanaohusika na sherehe za harusi za aina hiyo.
Rais huyo wa Gambia ametoa wito wa kuidhinishwa kisheria kwa marufuku hiyo baadae mwezi huu.
Post a Comment
Powered by Blogger.