POLISI KUKAMATA PEMBE 666 ZA NDOVU.Polisi nchini Tanzania wamekamata pembe 666 za ndovu zenye uzani wa tani 1.2 na thamani ya shilingi biloni 4.6 pesa za Tanzania sawa na dola milioni 1.2.
Mkurugenzi wa idara ya jinai bwana Diwani Athumani, amesema kuwa wageni wawili ni miongoni mwa watu 9 waliokamatwa katika operesheni hiyo.
Operesheni hiyo iliyohusisha maafisa wa polisi wa kimataifa kutoka Harare, Zimbabwena Nairobi, Kenyailifanikiwa kupata genge la watu 43.
''operesheni ‘Usalama III’ ilianza juni tarehe 26 hadi tarehe 30 na ilihusisha maafisa kutoka mataifa 26 barani Afrika waliokuwa na jukumu la kupeleleza na kunasa genge lililohusika na uwindaji haramu''. alisema Athumani.
''Tulifanikiwa kuwanasa walanguzi hao pamoja na wawindaji haramu 256 pamoja na bidhaa zao zilizotengenezwa kwa pembe za ndovu''
Vile vile tulifaulu kukamata mihadarati kama vile heroine, bhangi, miraa mbali na silaha kali ikiwemo bunduki 12 na risasi 104'' alisema bwana Athumani.
''tutatoa bidhaa hizi zote kama sehemu ya ushahidi wa polisi mahakamani aliongezea kusema bw Athumani.
Athumani aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa washitakiwa watafikishwa mahakamani karibuni.
Post a Comment
Powered by Blogger.