PIGO TASNIA YA HABARI,KIFO CHA MWANDISHI.


Tasnia  ya Habari nchini juzi ilipata pigo baada ya kuondokewa na Mwandishi wa Habari wa Michezo wa Kampuni ya Business Times Limited (BTL),inayozalisha Magazeti ya Business Times,Majira na Spoti Starehe, Elizabeth Mayambe.
Elizabeth Maybe ambaye aalikuwa Kaimu Mhariri wa Michezo Gazeti la Majira alikutwa na mauti juzi usiku akiwa nyumbani kwake Tabata kisukulu,Dar es salaam.
Kabla ya kukutwa na maui,marehemu alifanya kazi zake na majukumu yote ya kila siku bila kuonesha dalili za kuumwa.
Akiwa nyumbani kwake saa 2 usiku,alijisikia vibaya na kukimbizwa hospitali ya Amana,akiwa njiani alikutwa na mauti.
Kwa mujibu wa familia ya marehemu,Elizabeth Mayemba atazikwa kesho mkoani Morogoro kwenye Makaburi ya Kola.
Elizabeth Mayemba ataagwa leo kuanzia saa 5.00 asubuhi nyumbani kwake Tabata Kisukulu.bbada ya misa miili utasafirishwa kwenda Morogoro kwa mazishi.
Tania ya Habari imepata pigo kubwa kwa kuondokewa na Elizabeth Mayemba,ambaye alikuwa na mchango mkubwa kila mtu.
Marehemu ameacha mume na watoto watatu wa kiume.
Post a Comment
Powered by Blogger.