PICHA 8:Chama Cha Wasambazaji Wa Filamu Na Shirikisho La Filamu Waipongeza Serikali.
 Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Simon Mwakifamba,akizungumza na waandishi wa habari,Dar es Salaam,leo kuhusu kuipongeza serikali kupitia wizara husika katika kuanzisha oparesheni ya kuwakamata walanguzi wa kazi za wasanii nchini. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wasambazaji wa Filamu nchini,Moses Mwanyilu. Picha zote na Elisa Shunda


 Mwenyekiti wa Chama cha Wasambazaji wa Filamu nchini,Moses Mwanyilu,akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo.


 Waandishi wa habari wakimsikiliza mwenyekiti wa chama cha wasambaji wa filamu nchini,Moses Mwanyilu (hayupo pichani) wakati akizungumza nao kuhusu wizi wa ulanguzi wa kazi za wasanii nchini.


 Katibu wa Chama cha Wasambaji wa Filamu Tanzania,Suleiman Ling'ande,akizungumza katika mkutano huo.


 Muigizaji wa Filamu za Bongo Movie nchini,Kulwa Kikumba Al maarufu Dude,akitoa ufafanuzi katika mkutano huo juu ya athari za uharamia wa kazi za wasanii ambapo alisema kuwa wasanii nchini wanakuwa maskini wa kutupwa kutokana na wizi wa kazi zao ambapo wao huzifanya kwa fedha nyingi lakini faida hakuna na kazi hizo kuwatajirisha watu wachache ambao wanadurufu kazi hizo za wasanii na kwenda kuzitandaza mitaani kwa kuuza shilingi 1000 na kuisababishia hasara serikali kwa kutolipa kodi kwa mamlaka ya mapato nchini (TRA) kwa kutoweka stempu.


Post a Comment
Powered by Blogger.