PICHA 7:FUNGATE YA MTU MMOJA.

Tafakari haya -kwa akina dada sana sana - kufanya harusi ya kufana, lakini wakati wa kwenda fungate kufurahia mahaba ya ndoa mpya, mumeo anakosa kusafiri nawe...!
Je, utafanya nini?
Utaonyesha vipi kuwa unamkosa mpenzio?.

Hilo ni tatizo lilowasibu wanandoa wawili kutoka Pakistan, Huma Mobin na Arsalaan Severwa, waliofunga ndoa mapema mwaka huu.
Mpango wao ulikuwa kwenda fungate ya kukata na shoka nchini Ugiriki, japo maafisa wa ulinzi mpakani walikuwa na mipango mbadala!
Baada ya kulipia safari yao, Arsalaan alinyimwa cheti cha kusafiri yaani (visa) !
Ilimbidi Huma kusafiri bila mumewe, japo, aliandamana na mashemeji wake, baba na mama ya mumewe !
Lakini je, Huma alidhihirisha vipi kuwa anamkosa mumewe...?
Kwa kupiga picha kama amenyoosha mkono wake - ishara ya kumkumbatia mpenziwe - huku akiwa amekunja uso wake!
"kila wakati mmoja wetu anasafiri peke yake, huwa tunafanya hivyo kuonyesha kuwa tunakosana" . Huma ameambia BBC.
Picha hizo zilipigwa na mama mkwe wake ambaye wanauhusiano wa karibu sana.
Picha hizo zimesambaa mitandaoni kama moto nyikani !
Kwa sasa wawili hao wako pamoja mjini Lahore, wakitumai kuwa hatimaye watasafiri pamoja kuadhimisha mwaka mmoja wa ndoa yao!

Post a Comment
Powered by Blogger.