Nay Wa Mitego Ahofia BASATA Kuhusu Ngoma Mpya.

Nay wa Mitego amesema wimbo huo ‘Pale kati patamu’ anaamini utachafua
hali ya hewa tena kwa mashabiki kutokana na kile alichokiimba ndani ya
wimbo huo, kupitia ukurasa wake wa Instagram Nay wa Mitego alisema kuwa
akisikiliza wimbo huo yeye mwenyewe anapagawa yaani, na kuwataka
mashabiki kushika hiyo tarehe kwani watathibitisha wenyewe.
“Zimebaki siku kadhaa tu, Jumatatu Tarehe 11. Nitakua naachi wimbo wangu mpya. ‘Pale kati Patamu’ hii ngoma daaah mpaka napagawa yani. Shika iyo Tarehe na siku pale kati patamu sijui wataleta zengwe na hii?” aliuliza Nay wa Mitego
Nay wa Mitego kabla ya kuachia wimbo wake wa Saka hela, alitoa wimbo uliokuwa unafahamika kama ‘Shika adabu yako’ ambao ulifungiwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).