mwenyekiti wa usajili wa simba anena haya kwa Yangawww.seetheafrica.com
Laudit Mavugo


MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili wa klabu ya Simba, Zacharia Hans Poppe, amesema wanataka kuionesha Yanga jeuri ya fedha kwa kumsajili mkali wa mabao, Laudit Mavugo anayekipiga Vital’O ya Burundi.

Hans Poppe, alisema mazungumzo kati yao na uongozi wa Vital’O yanaenda vizuri na wana uhakika msimu huu mkali huyo atatua Msimbazi ili kurudisha heshima. “Hili ndiyo chaguo letu namba moja kwenye safu ya ushambuliaji inatokana na kipaji alichonacho,” alisema Hans Poppe.

Kiongozi huyo alisema wanataka kuwa na safu kali ya ushambuliaji ambayo kila shambulizi litakalofanywa na timu yao liwe na asilimia 85, kuzaa bao jambo ambalo litawahakikishia pia ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.

Alisema mbali ya Mavugo, tayari kuna wachezaji wengine wanaendelea kufanya nao mazungumzo kutoka Cameroon, Ivory Coast na Zimbabwe, ambapo anaamini watamalizana muda mfupi.

“Zipo taratibu tumejiwekea kama klabu, lengo letu ni kujenga timu imara itakayofanya vizuri katika kila mashindano tutakayoshiriki na kuacha kutoa visingizio kwa mashabiki, ndiyo maana tumekuwa makini sana kipindi hiki kwa sababu tusingependa kuona timu yetu ikifanya vibaya msimu ujao,” alisema.

Simba iliwahi kutangaza kumtaka Mavugo msimu uliopita lakini ilishindwa dau ilililokuwa imetangaziwa na klabu ya Vital’O anayoichezea.

Post a Comment
Powered by Blogger.