Mwasisi Wa Chadema Mtei:Ampongeza Rais Magufuli Na Kuzungumza Haya.

Mzee Edwin Mtei.

Mzee Mtei ametoa pongezi na kusema, Rais Magufuli ni kiongozi ambaye ameyatoa maisha yake ili kupambana kikamilifu na changamoto na pia matatizo ya Taifa yaliyosababishwa na uongozi mbovu katika usimamizi wa uchumi na raslimali nchini.
Amempongeza Rais Magufuli kwa kuwa kiongozi asiyependa mzaha katika kupambana na ruswa, ufisadi, uzembe na viongozi wabadhirifu wa mali za umma.

Mzee Mtei amemfananisha Rais Magufuli na Baba wa Taifa, Mwl. Nyerere katika kukabiliana na masuala ambayo ni changamoto na muhimu katika taifa.

Amemalizia kwa kusema ana furaha kuona Rais Magufuli anapambana kuhakikisha uchumi wa nchi unajengeka katika msingi imara kwa sababu viongozi wa nyuma wamejenga uchumi ambayo siyo endelevu kwa taifa.

''Rais Magufuli anatoa mwanga unaoonyesha makosa ya nyuma na nina furaha kuona Watanzania wanapewa tena nchi yao na kufufua viwanda vya ndani’’ Mtei alisema.

Kwa habari zaidi soma hii article katika gazeti la The Guardian on Sunday.
Post a Comment
Powered by Blogger.