MWANAUME NI NANI? [SIO MVULANA TAFADHALI].


MWANAUME NI NANI? (sio mvulana tafadhali).

Mwanaume ni sehemu ya uumbaji wa Mungu, ambae huanza majukumu katika umri mdogo kabisa.
Hutoa sadaka ndoto zake kwa ajili ya kuwafurahisha wazazi wake
Hutumia pesa yake aliyoipata kwa jasho kumnunulia zawadi mwanamke ampendae kwa ajili ya kumpa furaha.
Hujitoa ujana wake wote kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya mke wake na watoto wake bila kulalamika.
Hujenga future (kesho) ya watoto wake hata kwa kuchukua mikopo benki ambapo huilipa hata miaka yote.
Kamwe havai mlegezo, hasuki nywele, havai heleni wala kujinyonya nyonya midomo.
Kamwe hampigi mkewe, mkewe akikosea husuruhisha kwa njia za kidiplomasia na kwa akili. (kama maandiko matakatifu yalivyoagiza).
Mkewe akiwa katika majonzi na huzuni, humkumbatia na kumuangalia machoni, humwambia "mke wangu haya ni majaribu tu, nakupenda, usikate tamaa, mumeo nipo tutasonga mbele"
Mkewe na watu wengine hufikiria hivi juu yake;

Kama akienda out, basi si muangalifu.
Kama akibaki nyumbani, yeye ni mvivu.
Kama akiwagombeza wanae, ni mkali hajui kulea.
Kama asipowakaripia watoto, basi sio baba muwajibikaji.
Kama akimzuia mkewe kufanya kazi, basi ni mwanaume asiejiamini.
Kama asipomzuia mkewe kufanya kazi, basi ni mwanaume anaetegemea mshahara wa mkewe.
Kama akimsikiliza mama yake, basi ni mtoto wa mama.
Kama akimsikiliza mkewe, basi ni mtumwa wa mkewe au mume bwege.

**********

Muheshimu kila mwanaume anaekupenda kwa dhati, huwezi jua ni mangapi anajitahidi kuyafanya ili tu akupe furaha wewe.

Pia nakupa pole kama umeumizwa, aliyekuumiza sio.
 MWANAUME huyo ni MVULANA JOGOO, MWANAUME.

 kamwe hadondoshi chozi la Mwanamke wake, kwake mwanamke wake ni tunu na johari ambayo inapaswa kutunzwa na kuthaminiwa kwa hali na mali!.

"WANAUME" wa namna hii wapo, kama bahati mbaya haujawahi kukutana nae pole sana. Hiyo ilikuwa sample ndogo hivyo hauwezi ukathibitisha kuwa wote wako hivyo. Shuhuda ni nyingi mno.

Narudia tena pole sana, omba MUNGU, utakuja pata MWANAUME, au Omba Mungu ambadilishe huyo uliyefunga nae pingu au mtarajiwa wako kutoka Mvulana kuwa Mwanaume.
Post a Comment
Powered by Blogger.