MWANAUME AFUKUZA MKEWE KISA KUMBIKUMBI.Na Dorcas Safiel.

Mwanaume mmoja mjini Vihiga,magharibi mwa Kenya amewashangaza wanakijiji wa Munoywa baada ya kumfukuza mkewe nyumbani kwa kula kumbikumbi wake.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 24 kwa jina Lucas Luvai alimvamia mkewe baada ya kugundua amekula kumbikumbi wake wa kukaanga.
Kumbikumbi ni wadudu au chakula kinachoenziwa sana na watu wa kutoka magharibi mwa Kenya.
Jamaa huyo aliwanunua kumbikumbi kwa ajili ya chakula chake cha mchana kwa sababu mkewe huwa kazini wakati huo.
Hata hivyo mkewe aliporudi nyumbani na kusikia harufu nzuri ya kumbikumbi alishindwa kujizuia na kuwatafuna wote,jambo lililosababisha Lucas kumfukuza.
Hivi sasa Lucas anamuomba msamaha mkewe aliyemfukuza,kwani anadai alikuwa amelewa wakati wa tukio hilo.
Lucas anasema mkewe amekataa kumsamehe kwa sababu kila akimpigia simu hachukui.
Post a Comment
Powered by Blogger.