Mwanamuziki Na Mwigizaji Lady Gaga Aachana Na Mchumba Wake.

Mwanamuziki na mwigizaji mashuhuri kutoka Marekani Lady Gaga amefichua kwamba yeye na mchumba wake “wametengana” kwa muda.Ameandika ujumbe kwenye Instagram na kuwaomba mashabiki wawasaidie na kuwaunga mkono.
Lady Gaga na Taylor Kinney wamekuwa pamoja kwa miaka mitano lakini uvumi umekuwa ukienea kwamba urafiki wao umeingia kutu.
Amesema bado wanapendana sana lakini juhudi zao za kutaka kutimiza ndoto zao maishani, kuwa mbali pamoja na shughuli nyingi za kikazi vimetatiza uhusiano wao.
Lady Gaga, 30, alianza kuchumbiana na Taylor Kinney, ambaye ni mwigizaji na mwanamitindo, baada ya kukutana naye akiandaa video ya wimbo wa You and I mwaka 2011.
Alimchumbia Siku ya Wapendanao mwaka 2015, na akamvika pete ya almasi ya umbo la moyo.
Wawili hao hawajapigwa picha sana wakiwa pamoja siku za karibuni.
Gaga, ambaye jina lake halisi ni Stefani Joanne Angelina Germanotta, pia ameonekana mara kadha akiwa hajavalia pete ya uchumba.
Mashabiki wao huwaita wawili hao "Tayga", kutokana na majina yao Taylor na Gaga.
Baadhi ya mashabiki wamekuwa wakishangaa kuhusu hatima ya mbwa wawili wanaomilikiwa na wawili hao, ambao majina yao ni Koji na Miss Asia Kinney.
Post a Comment
Powered by Blogger.