Mwanamitindo Maarufu Afrika Mashariki Azungumzia Jinsi Alivyopoteza Usichana Wake.

Msichana maarufu Afrika na haswa Afrika Mashariki kwa uzuri wake aelezea alivyojisikia siku aliyopteza usichana wake. Japokuwa hakusema alipoteza usichana wake akiwa na umri gani, Huddah aliongelea tu alivyojisikia kuwa ni mkosaji mkubwa kwa kuwa mama yake alikua mkali sana.
“Huwa najiuliza siku zote, hivi wazazi hujua kwamba watoto wao wamepoteza bikira? kwasababu siku niliyopoteza yangu, nilijisikia kuwa ni mwenye makosa hadi hadi nikawa natetemeka kwa maana mama yangu alikua mkali sana”. aliandika hayo kwenye mtandao wa jamii wa Instagram.
Na kisha aliendelea kwa kusema kwamba tangu pale hakuwahi kabisa kumtazama mama yake machoni kwasababu alihisi mama yake tayari alifahamu kwamba mtoto wake amekuwa si mtoto tena.
Msichana huyu kutoka Kenya bila shaka anajulikana zaidi kwa muonekano wake mzuri wa kuvutia kimapenzi na post yake hii ilivutia watu wengi sana  wanaomfollow kwenye ukurasa wake instagram.
“Sikuwahi kuweza kumuangalia mama tena usoni kwasababu nilidhani aliweza kuona undani wangu, kiasi hata chakula nikawa nakula chumbani. nilidhani alijua na akaamua tu kukaa kimya kitu ambacho ndo kilizidi kuniua. Sikuwahi kukaa nae kwenye meza moja ya chakula mpaka kama miaka 2 iliyopita……Hivi wazazi huwa wanajua? hivi alitambua kama sikua mtoto wake tena? bado hili linaniumiza” 
sidedhuu

Post a Comment
Powered by Blogger.