MTOTO WA MIAKA 4 AKUTWA AMEFARIKI KWA KUNING'INIZWA. Mtoto wa kike, Rahila Salim Ali (4) amekutwa amekufa huku mwili wake ukiwa umening’inizwa kisimani na vidole vya mikono vikiwa vimekatwa na mashavu kuchubuliwa. Tukio hilo limetokea jana asubuhi katika eneo la njia panda mbagala baada ya mtoto huyo kutoroka nyumbani baada ya siku nne zilizopita.

Mama mzazi wa mtoto huyo alisema binti yake alitoweka nyumbani saa tano asubuhi wakati wakiwa wanaangalia television kitu ambacho hakikuwapa wasiwasi na muda wa saa moja wakaaza kupata wasiwasi na kuaza kumtafuta, Aliongeza kuwa walitoa taarifa na baadhi ya vyombo vya habari bila mafanikio hadi jana mwili wake ulipokutwa umening'inizwa kwenye kisima cha nyumba ya jirani yao.
 " Nilipofika nilishangaa kuona nguo zake ni kavu na ana majeraha" alisema.

Pia alisema kuwa kisima hicho kina tundu dogo huenda wauaji walijitahidi kuusukumiza mwili huo ili ionekane kama amefia humo ikashindikana ,mpaka juzi mchana kilikuwa kikitumika na huenda mwili huo ulining'izwa usiku wa kuamkia jana.

Baadhi ya majirani waliliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina na kuwachukulia hatua watu ambao walikuwa wakijihusisha na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.
 Kamanda wa Temeke,Andrew satta alisema wanaendelea na uchunguzi "Taarifa zilizopo ni kwamba amekufa maji lakini kwa hayo mazingira mengine tunaendelea kufanya uchunguzi zaidi".
Post a Comment
Powered by Blogger.