MTIBWA NI SHAMBA LA BIBI LINALOPOTEZA MABILIONI.

MTIBWA NI SHAMBA LA BIBI LINALOPOTEZA MABILIONI.

Mtibwa Sugar ni moja ya klabu inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara kwa zaidi ya muongo mmoja sasa, ikiwa imewahi kuchukua ubingwa mara mbili na haijawahi kushuka daraja tangu ilipopanda.

 Ni klabu inayojulikana kwa kutoa mchango mkubwa wa vipaji kwenye soka la Tanzania kwa muda sasa. Naiangalia Mtibwa kama vile klabu za Southampton, fc Porto, Ajax Amsterdam, Genk nk ambazo zina historia ya kutoa mchango wa vipaji vya soka ktk ligi mbali mbali huko barani Uropa.

 Mtibwa Sugar ni shamba la vipaji ambalo kila msimu wa soka unapomalizika basi wenye mahitaji hujiendea kuvuna. Bila kujali misimu iliyopita, nauangalia msimu ulioisha na wakati huu tukiwa kwenye usajili tayari jina Mtibwa linatajwa sana ktk harakati za usajili si kwa kutwaa wachezaji bali kutoa.

 Majina kama Andrew Vicent, Shiza Kichuya, Mohamed Ibrahim, Muzamir Yacine nk yanatajwa sana katika harakati hizi za usajili.

 Swali kubwa ninalojiuliza, Mtibwa inafaidikaje na usajili huu? Swali hili ndilo linalonifanya niione Mtibwa kama shamba la bibi ambalo mmiliki wake hajajua thamani ya mali iliyomo humo. 

Nawaangalia wachezaji wanne niliowatolea mfano hapo juu wakiondoka na zaidi ya sh mil 100, za Mtibwa. Kwa hesabu za haraka haraka nawathaminisha hawa wachezaji km ifuatavyo:- 

1. Andrew Vincent-mil 25 2. Shiza Kichuya-mil 30 3. M'med Ibrahim-mil 20 4. Muzamir Yacine-mil 20 Haya si mahesabu halisi ni ya kubuni kwa kuzingatia nafasi zao, umuhimu nk. Lakini kwa nn Mtibwa haijapata chochote au kama wamepata haijulikani? Klabu zetu zinaposainisha wachezaji huangalia msimu mmoja tu wa ligi, na wachezaji hawachukuliwi kama sehemu ya kitega uchumi cha klabu.

 Ndiyo maana mikataba ya vilabu vyetu huwa si zaidi ya miaka miwili na haina vipengele muhimu kama "release clause".

 Endapo Mtibwa wangejifahamu kuwa ni shamba linalotoa mavuno yanayowindwa kila msimu bila shaka wangekuwa wanavuna zaidi ya mil 100 kila msimu. Lakini nani analitambua hili na kuliwekea mkakati maalumu ili Mtibwa inufaike na kuwa mfano kwa klabu zingine? Shamba la bibi linalopoteza mabilioni ktk soka la bongo.

 ‪#‎Imani‬ K Mbaga
Post a Comment
Powered by Blogger.