Mke Wa Donald Trump Afuta Tovuti Yake.

Mke wa mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donal Trump, Melania, amefuta tovuti yake baada ya vyombo vya habari nchini Marekani kuanza kutilia shaka ukweli wa baadhi ya madai yake.
Bi Trump amesema tovuti hiyo imefutwa kwa sababu haikuwa inaashiria wala kuonyesha mambo anayoangazia kwa sasa.
Vyombo vya habari nchini Marekani vilikuwa vimetilia shaka ukweli wa madai kwamba ana shahada katika usanifu mijengo kutoka chuo kikuu kimoja nchini Slovenia, kama alivyokuwa ameandika katika wasifu wake mtandaoni.
Kitabu kuhusu maisha yake kilichochapishwa mwaka huu kinasema aliacha masomo baada ya mwaka mmoja kuangazia kazi ya uanamitindo.
Wiki iliyopita, Melania Trump, alishutumiwa vikali baada ya hotuba aliyoitoa kwenye Kongamano kuu la chama cha Republican, kudaiwa kuwa kukopa sana maneno kutoka kwa hotuba iliyotolewa na mke wa rais wa sasa Michelle Obama katika kongamano la chama cha Democratic miaka minane iliyopita.
Post a Comment
Powered by Blogger.