MH.GONDWIN GONDWE AZUNGUMZIA KUHUSU MADAWATI.
  Mkuu mpya wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe ametoa vipaumbele vyake vya awali kwa wakurugenzi na watumishi wa wilaya hiyo akiagiza vifanyiwe kazi haraka ili kuleta ufanisi katika kazi na maendeleo ya eneo hilo.
Akizungumza na viongozi hao jana katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi amesema ameshaona mambo yanayotakiwa kufanyiwa kazi kwa haraka zaidi ili kupata maendeleo.
Gondwe amesema suala la madawati linatakiwa kukamilika kwa haraka huku akiwataka wakurugenzi wampe ushirikiano pale walipoishia.
Post a Comment
Powered by Blogger.