MAJIBU YA CCM BAADA YA CHADEMA KUTANGAZA SIKU YA MAANDAMANO NCHI NZIMA YAPO HAPA.

Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka.
Msemaji wa chama cha mapibduzi CCM bw.Christopher Ole Sendeka ameongea na waandishi wa habari  na kuzungumzia hatua ya chama cha Chadema kufanya maandamano ya nchi nzima.
Sendeka alisema kuwa jana tarehe julai 27 chama cha Chadema walitoa kaulizilizojaa uongo mwingi za kibabaishaji na kuthibitisha ukweli kuwa kwa hakika kutokana na kasi ya serikali ya Rais John Pombe Magufuli na kufanya wapinza kukosa pointi za kuongea.
''Katika uongo na uzushi waliotangaza wapinzani yaani chama cha Chadema wameamua kufanya mikutano na maandamano nchi nzima,kwa hoja walizoeleza zimejaa uongo na upotoshaji uliokithiri ikumbukwe kuwa serikali haijazuia mikutano kwenye majimbo yao''alisema Sendeka 
''Wabunge wako huru kufanya kazi zao  na tumeshudia wabunge wakifanya kazi zao katika majimboni bila wasiwasi wakiwemo hao Chadema au Ukawa.
''Turudi nyuma kuwa matukio kwenye mikutano hii au operesheni kama hizi yalipoteza maisha ya vijana wetu na matokeo ya kila mikutano ya holela''alisema Sendeka
Post a Comment
Powered by Blogger.