Maiti Yazuiliwa Muhimbili Ikidaiwa Fedha.

Hospitli ya Taifa Muhimbili imegoma kuruhusu mwili wa marehemu Bi.Hilda Lukas mwenye miaka 30 aliyefariki dunia juni 26 katika hospitali hiyo,aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa utumbo kutoboka huku ikidai lazima fedha zote wanayomdai marehemu ilipwe ambayo ni sawa na shilingi milioni moja na laki moja na nusu kwa mujibu wa ndugu wa familia kama gharama za kumuhudumiamgonjwa huyo.
Mama wa marehemu Bi.Anna Zuaro na Bibi wa marehemu wameiomba serikali na wadau mbalimbali kuona namna ya wanavyoweza kuwasaidia kwani wao mpaka sasa hawana fedha za kuuondoa mwili wa mpendwa wao,huku gharama za kuuhifadhi mwili huo katika chumba cha kuhifadhi maiti zikizidi kuongezeka.
Kwa Maafisaa wa Muhimbili wanakiri marehemu Hilda Lukas alikuwa amelazwa katika wodi ya Kibasira chumba namba 9 ingawa haikuwa rahisi kuzungumza na maafisa hao.
Uongozi wa Chang'ombe umesema umefanya juhudi nyingi tu zikiwemo za kuchangisha wananchi na wadau mbalimbali lakini mpaka sasa bado hawajaweza kukamilisha kiasi hicho cha fedha kinachohitajika Muhimbili ambapo gharama za Mochwari pekee mpaka sasa ni shilingi 210,000.

Source:ITV.
Post a Comment
Powered by Blogger.