KITUO CHA DOKTA MWAKA CHAFUNGIWA.Serikali imekifungia kituo cha tiba asilia cha Foreplan kinachomilikiwa na Juma Mwaka kwa kukiuka masharti ya kibali alichopewa kujitangaza kuwa anatoa tiba za kisasa badala ya matibabu ya asilia.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mwenyekiti Wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Dk Edmund Kayombo amesema kuwa kituo hiko kimefutiwa usajili na hakiruhusu kutoa huduma za tiba asilia na tiba mbadala kwa jamii kwa kutokidhi masharti ya usajili na kufanya kazi kinyume cha usajili wake.
Post a Comment
Powered by Blogger.