Kampuni Ya Tigo Kusimamia Mpango Mzima Wa Fiesta 2016.

Dar es salaam Julai 14, 2016 kampuni ya tigo imetangaza kuwa itakuwa mdhamini mkuu wa tamasha la Fiesta 2016 ambalo huvutia umati mkubwa wa watu kutoka sehemu mbalimbali nchini.
akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamasha hilo , ofisa mkuu wa biashara wa tigo shavkat berdiev alisema ’ ikiwa ni Kampuni iliyojikita katika kukuza sekta ya muziki wa ndani tunayo furaha kuwa wadhamini wakuu wa tamasha hilo kubwa kukuza wasaniiwa ndani kupitia majukwaa ambayo yatawezesha kuonesha vipaji vyao kulinganisha na mashabiki ili kuzipaisha kazi zao na kufanikiwa kupata kiasi kikubwa cha fedha.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mkurugenzi mtendaji , mtengaji wa prime time promotions Joseph Kusaga alisema “ tutaendelea na harakati zetu za kuendeleza vipaji kutoka kwa wasanii wapya na wanaoibukia katika kizazi kipya wakati wa tamasha la fiesta 2016 kama ambavyo tulifanya awali wakati wa tamasha la Dance la Fiesta , Fiesta super star na bonanza la soko la Fiesta.
amegusia pia idadi ya wasanii imeongeza kwa kiwango kikubwa hapa nchini na matokeo ya hali hii ni kwamba prime time promotions inawabaini wasanii wanaojishughulusha katika vikundi mbalimbali vya tamadunika ili kushirikia katika hili na tutawaelimisha wasanii bila kuchoka kupitia semina kadhaa ili kubadilisha muziki kuwa moja ya biashar na kuibua fursa zaidi za ajira kwa makundi mengine.
Post a Comment
Powered by Blogger.