Kambi Kuu Ya Wanajeshi Yavamiwa.

Washambuliaji wa kujitoa mhanga wameshambulia kambi kuu ya wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika (AU) mjini Mogadishu.
Milipuko miwili mikubwa imesikika na baadaye kukatokea ufyatuaji wa risasi.
Makao makuu ya wanajeshi hao yamo karibu na uwanja wa ndege wa Mogadishu, eneo ambalo pia lina afisi nyingi za ubalozi za mataifa ya Magharibi na Umoja wa Mataifa.
Shirika la habari la Reuters linasema watu saba wamefariki.
Kundi la al-Shabab limedai kuhusika, na kusema watu zaidi ya 12 wameuawa kwenye shambulio hilo.
Post a Comment
Powered by Blogger.