KABLA YA KUAHIRISHA BUNGE WAZIRI MKUU ASEMA NENO.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Na Dorcas Safiel.

Jana bungeni Dodoma wakati wa kuhairisha bunge hadi septemba mwaka huu Waziri mkuu wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa alisema kuwa serikali haijaminya demokrasia ndani ya bunge kama inavyoelezwa na wabunge wa chama cha upinzani na kinachoonekana ni kutokuwa na ukomavu  wa kisiasa.
 Pia aliongeza kuwa kitendo cha wabunge kususia vikao vya bunge haitoi picha nzuri kwa wananchi walio wachagua kwani haisuruhishi matatizo  na akatoa rai kuwa waheshimiwa wabunge hao wanabidi watafakari upya uamuzi wao na kuwasihi kutafakari upya uhamuzi wao na kuwasihi kuingia bungeni ili kwa pamoja na ushirikiano waweze kutoa ushauri kwa serikali kwa maendeleo yao wananchi wote.
Post a Comment
Powered by Blogger.